Thursday, January 21, 2016

UJUMBE MUHIMU KWA WEWE ULIYEPONYWA NA YESU KUPITIA HUDUMA HII.


Kwa kuwa sasa yesu amekuponya.
Jua kuwa:-
i.MUNGU amekuponya ili umfuate yeye kwa kumkubali YESU aweze kukuokoa nawe uwe mwaminifu hata mwisho wa maisha yako naye ndipo atakavyo kuokoa na moto wa milele kama alivyokuokoa katika ugonjwa wako.
Je una mfuataje YESU?.Ni  kwa kutii kila agizo lake unalolisikia kupitia watumishi wake katika huduma hii, kwa kuhudhuria kanisani na katika mafundisho ya vipindi mbali mbali katika kanisa lililo hai.
ii.MUNGU amekuponya ili umtumikie umtumikie kwa njia mbalimbali kama vile:-
a.       Kuchangia gharama mbalimbali za huduma.
b.      Kuwaambia watu wenye shida kama uliyokuwa nayo habari za kuponywa kwako ili nao waje kupokea uponyaji wao kama wewe ulivyopokea uponyaji wako.
c.       Unaweza kumtumikia MUNGU kwa vipawa vyako kama vile uimbaji.
iii.MUNGU amekuponya ili uwe shuhuda kwa watu wengine wanaopitia tatizo kama ulilokuwa nalo.Sasa anza kushuhudia wengi zaidi juu ya kuponywa kwako naye MUNGU atapendezwa zaidi nawe naye atakubariki zaidi na zaidi.
Kwa mawasiliano ya huduma hii piga simu no: 0714 409256 au email:wwc4all@gmail.com
 Au tembelea blog yetu:www.wabarikiwa.blogspot.com, Facebook:WWC MOKOZI