Kwa kuwa
sasa yesu amekuponya.
Jua kuwa:-
i.MUNGU
amekuponya ili umfuate yeye kwa kumkubali YESU aweze kukuokoa nawe uwe
mwaminifu hata mwisho wa maisha yako naye ndipo atakavyo kuokoa na moto wa
milele kama alivyokuokoa katika ugonjwa wako.
Je una mfuataje YESU?.Ni kwa kutii kila
agizo lake unalolisikia kupitia watumishi wake katika huduma hii, kwa
kuhudhuria kanisani na katika mafundisho ya vipindi mbali mbali katika kanisa
lililo hai.
ii.MUNGU
amekuponya ili umtumikie umtumikie kwa njia mbalimbali kama vile:-
a.
Kuchangia gharama mbalimbali za huduma.
b.
Kuwaambia watu wenye shida kama uliyokuwa nayo
habari za kuponywa kwako ili nao waje kupokea uponyaji wao kama wewe
ulivyopokea uponyaji wako.
c.
Unaweza kumtumikia MUNGU kwa vipawa vyako kama
vile uimbaji.
iii.MUNGU amekuponya ili uwe shuhuda kwa watu wengine
wanaopitia tatizo kama ulilokuwa nalo.Sasa anza kushuhudia wengi zaidi juu ya
kuponywa kwako naye MUNGU atapendezwa zaidi nawe naye atakubariki zaidi na
zaidi.
Kwa mawasiliano ya huduma hii
piga simu no: 0714 409256 au email:wwc4all@gmail.com
Au tembelea blog yetu:www.wabarikiwa.blogspot.com, Facebook:WWC MOKOZI
No comments:
Post a Comment