ISAYA 1:3 “Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali
Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.”
MUNGU anapendezwa na watu wenye kujituma kufikiri na kuelewa vizuri
utendaji wake.
YEREMIA 1:11-12 “Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia, waona
nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.
12 Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa
maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.”
MUNGU anampima Yeremia kama ana umakini sawa sawa kwa kumuuliza
anachokiona !,
Na akagungua kweli anaumakini sawa sawa baada ya Yeremia kujibu kisahihi
kile anachokiona.
MUNGU huwa anatupa uwezo mkubwa lakini tatizo huwa ni uvivu,ulegevu,kujisahau,kutojali
, wepesi wakukata tamaa nazo huzaa
*Kuchelewa kanisani
*Kujisikia uvivu kuomba na kusoma neno kila siku.
*Kupuuzia ujumbe wa MUNGU na tabia nyingi nyingi mbaya ambazo zina
sababisha kupunguza nguvu ya MUNGU ndani yetu.
MUNGU anaweza kuwa amekupa nguvu na ukawa hauitumii ,au amekupa akili na
hauitumii kisawa sawa ,sasa ni wakati wa kujitenga na makosa yote na kuamka
kutumia kila tulichopewa na MUNGU kwa MAKINI na WEREVU kwa ajili ya utukufu wa
MUNGU.
MATHAYO 25:1-12 “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali
kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye
busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae
na mafuta pamoja nao;
4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo
vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala
usingizi.
6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana
arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza
taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni
mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo;
hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao,
mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi
akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema,
Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui
ninyi.”
Kutokuwa
na Busara ,uhodari ,hekima,maarifa,bidii,umakini na uwerevu kunaweza
kukukosesha mbingu hivyo anza leo kuwa navyo hivyo vyote.
Kubali
kubadilika pia muombe MUNGU kila siku na
akufanye uwe makini zaidi katika maisha yako.
No comments:
Post a Comment