2 SAMWELI 15:31 -“Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao
waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la
Ahithofeli liwe ubatili.”
Katikati
ya vita kubwa au matatizo mengi yana yokukumba kwanza jifunze kukiri USHINDI tamka NENO zuri katikati ya taarifa
mbaya naye MUNGU ataangalia neno lako ili alitimize vile vile kama
ulivyolisema.
Daudi
aliijua siri hiyo na ndiyo maana alipoletewa taarifa mbaya kuwa Ahithofeli naye
amemuasi hapo hapo alimsihi BWANA kugeuza shauri lake na kweli lileshauri baya
la Ahithofeli MUNGU alilibadilisha.
2 SAMWELI 17:1-14 -“ …………………..5 Ndipo
Absalomu akasema, Basi, mwiteni Hushai, Mwarki, naye, tukasikie atakayosema
yeye pia.
6 Basi Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu
akamwambia, akasema, Ahithofeli amesema hivi; je! Tufanye kama alivyosema? Kama
sivyo, sema maneno yako.
7 Hushai akamwambia Absalomu, Shauri hili alilolitoa
Ahithofeli si jema wakati huu.
8 Hushai akafuliza kusema, Wamjua baba yako na watu
wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama
dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita,
hatalala pamoja na watu wake.
9 Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo;
kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia,
atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu.
10 Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa
simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni
shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa.
11 Kwa hiyo shauri langu ni hili, Waisraeli wote toka
Dani mpaka Beer-sheba wakusanyike kwako, kama mchanga wa bahari kwa wingi; na
wewe uende vitani mwenyewe.
12 Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na
kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja
wao, yeye na watu wote walio pamoja naye.
13 Tena, ikiwa amejitia katika mji uwao wote, basi
Israeli wote wataleta kamba, na kuuendea mji ule, nasi tutaukokota mpaka mtoni,
wala halitaonekana huko hata jiwe dogo moja la mawe yake.
14 Naye Absalomu na watu wote wa Israeli
wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa
maana Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili Bwana
alete mabaya juu ya Absalomu.”
Kuna
vitu vingi ambavyo BWANA anasubiri neno lako
na usihi wako kwake ili avitimize !.
Jifunze
na ujizoeshe kubadilisha taarifa zote mbaya za maisha yako kwa kukiri vizuri
kwa kutegea jina la BWANA na utashangaa tuu MUNGU anafanya vile vile kama
ulivyosema.
BY PROPHETESS
Tumaini