YOHANA 8:3-11 “Waandishi
na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka
katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa
alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe
wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu
ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye
asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake
katika nchi.
9 Nao
waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia
tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke
amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke,
akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu
kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu
akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”
Kutoka kwenye huo mstari juu YESU anatuelekezea vitu viwili navyo ni cha kwanza ni kuwa hakuna mwanadamu
mwenye hadhi/kiwango cha kuhukumu mweziwe na jambo la pili
ahukumuvyo MUNGU ni tofauti na wanadamu.
Ahukumuvyo MUNGU ni tofauti sana na mwanadamu kwa wanadamu waliona
sahihi mwanamke huyo kuhukumiwa kwa kumpiga kwa mawe kama ilivyo desturi lakini
kwa upande wa MUNGU haikuwa sahihi
kupigwa mawe bali KUSAMEHE.
Yule mchawi ambaye wewe unamuombea afe lakini MUNGU anampa nafasi zaidi
kwa kumuhurumia akitegemea yamkini siku moja atatubu ili amuokoe.
Je wewe ni wangapi leo ambao umewahukumu au umeshawanenea mambo mabaya?,
Inatakiwa utubu na kumuomba msamaha MUNGU kwa ajili ya wote ambao uliwahukumu
kwa kuwa Imeandikwa Luka 6:37 “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi
mtaachiliwa.”
Watu wengine wamekuwa wakihukumu hata watumishi wa MUNGU pasipo kujua kuwa MUNGU
hapendezwi na mtu yeyote kumuhukumu mwenziye na pasipo kujua kuwa hukumu yao
sii ya MUNGU na hukumu ya MUNGU ndiyo pekee ya haki.
Hesabu 12:1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa
amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
Hapo tunaona miriamu na haruni wakimsema MUsaa na MUNGU hakupendezwa nao
hata kidogo.
Wajibu wetu kama wakristo ni kuwaombea yeyote Yule aliye na kosa na sii
kumhukumu kwa kuwa lile tulionalo ni kosa kwetu kwa MUNGU linaweza lisiwe kosa..
HESABU 12:7-10 “Sivyo
ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala
si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa
Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
9 Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale
juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni
akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.”
Mungu aliwaadhibu kwa kumsema mtumishi wake.
Yule ambaye wewe unamuhukumu kwamba ni mchafu sana !?,MUNGU hamuhukumu
hivyo bali anamhurumia na kumzidishia siku akitegema yamkini siku moja atatubu
dhambi zake
Mungu hakati tama na mtu yeyote na hapendi sisi tuhukumu wengine
Sasa nawe badilika na kuwa na mtazamo wa ki MUNGU sahihi kwa kutohukumu
yeyote bali kumuhurumia na kumuombea rehema yeyote unayemuhisi anahitaji
hukumu.
USIHUKUMU YEYOTE anayekosa BALI funga na kuomba kwa ajili yake na MUNGU
atambadilisha na kwa kufanya hivyo MUNGU atapendezwa na wewe sana.
No comments:
Post a Comment